Serikali ya Italia yaahidi kuisaidia Tanzania kwenye ujenzi wa barabara na ukarabati wa hospitali ya Ipamba iliyopo Iringa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga yupo nchini Italia kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Italia (Italy – Africa Ministerial Conference) uliofanyika tarehe 18 Mei 2016 katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo masuala mengi ya ushirikiano kati ya Afrika na Italia yalizungumzwa. Kati ya masuala hayo ni pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo na nishati na namna zinavyoweza kuinua uchumi wa nchi za Afrika.
Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichangia mada kwenye mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Italia