tanzania
bendera

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mipango ya Chakula Duniani (WFP) na balozi Madafa

Tarehe 13 Februari 2019, Mheshimiwa Balozi Madafa alionana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mipango ya Chakula Duniani (WFP) ofisini kwake  alipokwenda kumkabidhi Hati za Utambulisho. Miongoni mwa mambo waliyoyajadili ni WFP kuendelea kununua Chakula kutoka Tanzania kama walivyofanya mwaka jana.

 Mkutano wa Italy afrika Oktoba 2018

Tarehe 24 na 25 Oktoba 2018, jijini Rome kulikuwa na Mkutano wa Italya-frika ambao ulihudhuriwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga na Mheshimiwa Balozi Madafa. Mkutano huo ulihusu mahusiano ya Kuchumi kati ya Italy na nchi za Afrika. Pichani Mheshimiwa Waziri Mahiga anaonekana akijadili jambo na baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo.

 

 Mabalozi wawili wa hiari wa Utalii nchini Italy

Kwa jitihada za Mheshiwa Balozi George Madafa, Bodi ya Utalii Tanzania imetoa kibali cha kuwa na Mabalozi wawili wa hiari wa Utalii nchini Italy. Pichani wanaonekana Mabalozi hao ambao kulia kabisa ni Bi. Judith Mushi na wa tatu kulia ni Bi. Anna Mrio pamoja na Mheshimiwa Waziri Mahiga. Ubalozi hushirikiana na Mabalozi hao wa hiari katika kuitangaza Tanzania na kuitafutia watalii.

 

 Kamishna Mkuu wa Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini  ndugu Rogers Siyanga

Tarehe 13 Desemba 2018, Kamishna Mkuu wa Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini  ndugu Rogers Siyanga alifika Ubalozini alipokuwa nchini Italy kwenye mafunzo ya muda mfipi. Pichani anaonekana Bwana Siyanga na mtaalamu aliyefuatana naye walipofika Ubalozini kumsalimia Mheshimiwa Balozi Madafa.

 

 Rambirambi MV Nyerere Balozi wa Burundi nchini Italy

Balozi wa Tanzania nchini Italy ana ushirikiano mzuri na Mabalozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika  (SADC). Katika kudhihirisha ushirikiano huo mzuri, pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi wa Burundi nchini Italy  Bibi Nisubile,  akiwa  ni mmoja kati ya Waheshimiwa Mabalozi wengi waliofika Ubalozini kusaini kitabu cha rambirambi wakati wa ajali ya MV Nyerenyere Kisiwani Ukerewe.

 

 Mh Japhet Hasunga Waziri wa kilimo na Chakula

Tarehe 13 na 14 February 2019 katika Makao Makuu ya Mfuko wa Maendeleo wa Kilimo Duniani (IFAD) kulikuwa na Mkutano wa Baraza la Magavana ambalo Mheshimiwa Japhet Hasunga - Waziri wa kilimo na Chakula alihudhuria. Pichani wanaonekana Mheshimiwa Waziri huyo, Mheshimiwa Balozi na msaidizi wa Waziri wakati wa Mkutano huo. Mheshimiwa Waziri pia alipata fursa ya kutembelea Makao makuu ya Shirika hilo ambako alijulishwa kwamba Tanzania imetengewa Dola Milioni hamsini na nane za maendeleo ya Kilimo katika kipindi cha miaka cha miaka mitatu ijayo.

 

 Kampuni ya Protcno ambayo imeunda Mitambo ya kutolea chumvi kwenye Maji

Tarehe 01 Machi 2019, Balozi aliwatembelea wamiliki wa Kampuni ya Protcno ambayo imeunda Mitambo ya kutolea chumvi kwenye Maji iliyoagizwa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Morogoro (MOROWASA) kwa ajili ya kufungwa katika mji wa Gairo.

 

 Kampuni ya Protecno

Pichani ni Mheshimiwa Balozi George Madafa akiwa na wamiliki wa Kampuni ya Protecno ambao ni Bwana Lorenzo Belbusti na Bwana Jacopo Belbusti. Kampuni hiyo hutengeneza Mitambo ya kuondolea chumvi kwenye Maji.

 

 Balozi akikagua mmoja kati ya Mitambo mitatu (3) ya kuondolea chunvi kwenye Maji

Mheshimiwa Balozi akikagua mmoja kati ya Mitambo mitatu (3) ya kuondolea chunvi kwenye Maji iliyotengezwa na Kiwanda cha Protecno kwa ajili ya Mji mdogo wa Gairo.

 

 Balozi wa Uganda nchini Italy Bibi Elizabeth Napoyek

Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Italy wamo katika maandalizi ya Mkutano wa uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Italy na wa nchi zao unaotarajia kufanyika mwezi April 2019. Pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Italy Bibi Elizabeth Napoyek wakijadiliana mipango ya Mkutano huo ofisini kwa Mheshimiwa Balozi Madafa.

 

 Balozi na kampuni ya TMT ya uzoaji wa kisasa wa taka ngumu

Mheshimiwa Balozi Madafa katika majadiliano na Kampuni iitwayo TMT iliyopo Ascoli Piceno Pwani ya Mashariki ya Italy  inayojihushisha na uundaji wa mabodi na matenki ya magari na pia uzoaji wa kisasa wa taka ngumu katika miji mikubwa. Kampuni hiyo inataka kuja kuwekeza nchini Tanzania. Pichani anaonekana Mheshimiwa Balozi Madafa na mwenyeji wake katika eneo hilo Bibi Anna Minja katika Mkutano wa kwanza na mwenye Kampuni hiyo Mhandisi  Alfredo Spinozzi wa tatu kutoka kushoto akiwa na wasaidizi wake Bi Daniela na Bwana Gino Lama. 

 

 Balozi Madafa katika majadiliano na Kampuni iitwayo TMT nchini Italia

 Mheshimiwa Balozi Madafa akiwa katika majadiliano na Kampuni ya TMT nchini Italia.

Most Popular

  • The Land of Kilimanjaro & Zanzibar Tourist's sites in Tanzania are indeed God sent gifts. Visitors to Tanzania do not only encounter the overwhelming force of nature but also enjoy a serene contact with it. They Read More
  • Investment Opportunities "Tanzania is no doubt, a great place to invest in Africa today. There are unlimited investment and business opportunities which you are invited to explore. For over the past decade Read More
  • Economic Diplomacy Economic considerations: Since the advent of the new millennium, economic considerations have received utmost priority in the formulation and conduct of Tanzania's foreign policy. The new foreign policy is geared Read More
  • 1
  • 2
  • 3