balozi madafa akisaini kitabu cha maombolezo ya rais moi
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Kahema Madafa akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Daniel arap Moi katika Ubalozi wa Kenya jijini Roma tarehe 6 Februari 2020.

Rais Mstaafu wa Kenya Mzee Daniel arap Moi alikuwa Rais wa pili wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002. Alikuwa Rais kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi wakati huo Mzee Jomo Kenyatta. Aliaga dunia akiwa kwenye matibabu katika hospitali ya Nairobi tarehe 4 Februari 2020 akiwa na umri wa miaka 95.