Balozi George MadafaKwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Watanzania wote wanaoishi na kufanya kazi nchini Italy na pia kwa niaba ya watumishi wote wa ubalozi wa Tanzania jijini Rome, mimi balozi George Kahema Madafa napenda kutumia fursa hii kueleza masikitiko yetu na huzuni tuliyo nayo kufuatia kifo cha mpendwa wetu Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Tunatoa pole kwa mama Janet na watoto pamoja na familia bila kuwasahau Watanzania wote kwa ujumla.

Tunaomba roho ya marehemu ikalazwe mahali pema peponi. Amina.


Balozi George Kahema Madafa

 

 

Matukio kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania mjini Rome

Jumamosi tarehe 20/03/2021 misa maalumu ya kumuaga rais Dkt. John Pombe Magufuli iliongozwa na baba askofu mkuu Protase Rugambwa ambayo ilifuatiwa na hotuba fupi ya balozi George Kahema Madafa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Italy Bw Abdulrahaman Koshi. Baada ya hapo wageni walitia saini kwenye kitabu cha rambirambi.

  |