Kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu J.K. Nyerere 1922-1999: Mwalimu afunika Roma!

Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbainiana kilichoko mjini Roma, hivi karibuni kilimtafakari Mwl. J.K. Nyerere 1922-1999: Fikra na mchango wake katika Jumuiya ya Kimataifa.

FRONTkumbukumbu ya miaka 20 kifo cha mwl nyere roma2

Katika hotuba yake, Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. George Kahema Madafa, alibainisha kwamba maisha, fikra na mawazo ya Mwl. Nyerere yamefumbatwa na uadilifu, bidii, usawa, mshikamano na uvumilivu usio na kipimo. Kama mtumishi wa serikali ya Tanzania, utendaji kazi wa Mwl. Nyerere ulisadifu kwa dhati fadhila na tunu msingi za maisha ya kikristo yaani; Imani, Matumaini na Mapendo kwa Mungu na unyenyekevu uliotukuka kwa watu aliowatumikia.

Chuo kikuu cha kipapa Urbaniana kupitia Kitivo chake cha Taalimungu kikishirikiana na Kitivo cha Misiolojia kilitenga siku ya alhamisi, tarehe 07 novemba 2019 kumtafakari Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwaalika viongozi na wataalamu mbalimbali kutoa hotuba zao.

Mengi soma zaidi kwenye makala maalumu ya Vatican News.